Saturday, January 5, 2019

Ndoa Ya Diamond na Tasha Mambo ni Moto Unaambiwa


Mambo ni Moto 
! Ndivyo unavyoweza kusema kwa sasa ndoa ya staa wa Muziki toka Tanzania, Nasibu Abdul a.k.a ‘Diamond Platnumz’ zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufunga Ndoa na bibi harusi mtarajiwa Tanasha Donna ‘Zahara Zaire’ akianika kufuru yake, Kupitia Gazeti moja la Udaku tumepata habari hizi nyeti
Kama unakumbuka siku chache za nyuma Diamond,alisema kuwa watafunga  ndoa yao mnamo Februari 14|2019 siku ambayo ni maalum kwa wapendanao na kama unakumbuka mwaka jana siku kama hiyo alipewa ua jeusi na aliyekuwa mpenza wake zari the Boss lady
TAARIFA KWANZA ZA NDUGU
Mitandao mbalimbali ya nchini Kenya ambayo imeeleza kupata taarifa za kufuru za ndoa hiyo kutoka kwa ndugu wa familia ya Tanasha na ndoa hiyo itakuwa ni ya kihistoria kwa mwaka huu 2019 kwani mbali na Diamond kuwa na jina kubwa na ukwasi wa kutosha, ndugu hao wa upande wa mwanamke nao si wepesi kihivyo.
“Tunajua Diamond amejipanga na anajimudu kifedha lakini na sisi huku kama familia hatuko vibaya sana. Tumejipanga vilivyo, wewe vuta picha mtu kama Diamond anafanya kufuru halafu na sisi tuongezee mzigo mezani itakuwaje?” alinukuliwa mmoja wa wanafamilia mtandaoni.
UNAAMBIWA WATU MAARUFU KIBAO
Mwanafamilia huyo alisema wanatarajia kuwa kwenye ndoa hiyo ambayo itakusanya watu wengi mashuhuri, kutakuwa na helkopta maalum ya kubeba maharusi, msafara wa magari kibao ya kifahari.